BODI YA MWAUWASA YAFANYA ZIARA DUWASA, IRUWASA NA MBEYA UWSA

Bodi ya Wakurugenzi ya Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Jijini Mwanza (MWAUWASA) imefanya ziara ya siku tano kwenye mamlaka tatu za maji ambazo ni Dodoma (DUWASA), Iringa (IRUWASA) na Mbeya UWSA lengo likiwa ni kujifunza na kubadilishana uzoefu.

Ziara hiyo ilianzia Mamlaka ya Maji Dodoma (DUWASA) na ilihitimishwa kwa kutembelea Mamlaka ya Maji Mbeya UWSA ambapo wajumbe walipata fursa ya kutembelea maeneo mbalimbali ya mnyororo mzima wa utoaji huduma ya maji ambayo ni kuanzia kwenye vyanzo vya maji hadi kwa mtumiaji wa mwisho.

Aidha, masuala mbalimbali yalijadiliwa kwa lengo la kubadilishana uzoefu na kutafuta ufumbuzi wa pamoja wa changamoto zinazozikabili mamlaka za maji nchini ili kufikia azma ya kupanua wigo wa usambazaji wa majisafi na salama kwa wananchi.

Kwa nyakati tofauti, katika majadiliano baina ya wajumbe wa MWAUWASA na wenyeji wao, ilipendekezwa mamlaka ziandae utaratibu wa kubadilishana uzoefu katika utekekezaji wa shughuli zao ili kuleta ufanisi zaidi hasa ikizingatiwa kwamba baadhi ya changamoto kwenye utekelezaji wa miradi ya maji kote nchini zinafanana.

Majadiliano hayo vilevile yaligusia suala zima la wizi wa mita za maji ambao umezikumba mamlaka nyingi nchini na huku baadhi ya mamlaka zikionyesha kufanikiwa kuliko zingine na hivyo ilipendekezwa watumishi wajikite katika suala hili ili kuona ni namna gani wengine wamefanikiwa.

Ziara hiyo ya Bodi ya MWAUWASA kwenye mamlaka hizo, vilevile ilihusisha baadhi ya watumishi wa MWAUWASA kutoka vitengo mbalimbali ambao waliambatana na wajumbe wa Bodi.

 

1.Wajumbe wa Bodi na baadhi ya watumishi wa MWAUWASA walipotembelea chanzo cha maji cha Mzakwe Jijini Dodoma  wakimsikiliza mtaalam (hayupo pichani) akiwapatia maelezo ya shughuli zinazofanyika maeneo hayo.

 

2. Wajumbe wa Bodi ya wakurugenzi MWAUWASA walipotembelea tenki la kuhifadhia maji lililopo maeneo ya Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM) wakimsikiliza Mkurugenzi Mtendaji wa DUWASA, Mhandisi David Pallangyo (kulia). Kutoka kushoto ni, Edith Mudogo, Frank Masasi, Denisa Pagulla na Ellen Bogohe

 

3.Wajumbe wa Bodi na baadhi ya watumishi wa MWAUWASA walipotembelea chanzo cha maji cha Chemchemi ya Kitwiru Mkoani Iringa.

4. Wajumbe wa Bodi za Wakurugenzi MWAUWASA na IRUWASA wakiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya watumishi wa mamlaka hizo mara baada ya kukamilisha ziara ya kwenye maeneo mbalimbali ya mnyororo mzima wa huduma ya maji Mkoani Iringa.

 

5. Wajumbe wa Bodi za Wakurugenzi MWAUWASA na wenyeji wao Mbeya UWSA walipotembelea chanzo cha maji cha Ivumwe.

6. Wajumbe wa Bodi za Wakurugenzi MWAUWASA na wenyeji wao Mbeya UWSA walipotembelea chanzo cha maji cha Nzovwe. Wa tatu kutoka kushoto ni Mwenyekiti wa Bodi MWAUWASA, Christopher Gachuma.

 

 

 

7. Wajumbe wa Bodi za Wakurugenzi MWAUWASA na wenyeji wao Mbeya UWSA walipotembelea eneo la kutibu maji la Swaya Jijini Mbeya. Wa pili kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji MWAUWASA, Mhandisi Anthony Sanga.

 

Published on: Dec 3, 2018  09:04