Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji, Mhandisi Emmanuel N.M Kalobelo (katikati waliokaa) akiwa katika picha ya pamoja na washirika wa maendeleo wanaohusika na utekelezaji wa miradi ya maji kupitia Programu ya Uboreshaji wa Huduma ya Majisafi na Usafi wa Mazingira ijulikanayo kama LV WATSAN. Programu hii inatekelezwa katika Ukanda wa Ziwa Victoria na inahusisha Jiji la Mwanza, Miji ya Bukoba na Musoma, Miji Midogo ya Misungwi, Magu na Lamadi. Mkutano huo wa Siku Tano ulilenga kujadili na kutathmini hatua iliyofikiwa ya utekelezaji wa miradi ambayo inatekelezwa chini ya Ufadhili wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania pamoja na Benki ya Uwekezaji ya Ulaya (EIB) na Shirika la Maendeleo la Ufaransa (AFD)