UFAFANUZI WA BEI ZA MAJI NA TOZO ZILIZOIDHINISHWA NA EWURA KWA MAMLAKA YA MAJISAFI NA USAFI WA MAZINGIRA JIJINI MWANZA (MWAUWASA)

Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Jijini Mwanza (MWAUWASA) imeanza rasmi kutekeleza Agizo la EWURA la kutoza bei mpya za maji zilizofanyiwa mabadiliko kuanzia tarehe 01 Julai, 2019. Mabadiliko ya bei hizi mpya za Huduma ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Jijini Mwanza zimeanza kutumika mara tu baada ya kuchapishwa na kutangazwa kwenye Gazeti la Serikali – GN Namba 486/2019 (kwa lugha ya Kiingereza) na GN Namba 490/2019 (kwa lugha ya Kiswahili) la tarehe 28 Juni, 2019…..bonyeza hapa kwa ufafanuzi zaidi