How to pay your bill with CRDB Bank

JINSI YA KULIPIA BILI YA MAJI MWAUWASA KWA CRDB BANK

Hakikisha una salio la kutosha kulipa bili

1. Hakikisha unaenda benki na bili yako au uwe na kumbukumbu sahihi ya namba ya akaunti yako ya maji (Customer Reference No.) – kwa mfano Na. 99889.

2. Jaza “deposit slip” ya benki kwa kuandika kwa usahihi jina lililo kwenye bili yako ya maji na kiasi cha deni la maji linalodaiwa kwenye hiyo bili.

3. Mkabibidhi mpokea fedha wa benki (teller/cashier) “deposit slip” na kiasi cha fedha za malipo ya deni la maji.

NB. Unaweza kulipa bili yako ya maji bila usumbufu kupitia tawi lolote la benki ya CRDB popote ulipo nchini Tanzania.