News

Posted On: Jun, 15 2020

Bodi ya Nane ya Wakurugenzi yazinduliwa rasmi na Katibu Mkuu Wizara ya Maji, Prof Kitila Mkumbo Juni 11, 2020

News Images

UZINDUZI WA BODI YA WAKURUGENZI JUNI 11, 2020

Katibu Mkuu Wizara ya Maji, Prof. Kitila Mkumbo amezindua rasmi Bodi ya Nane (8) ya Wakurugenzi ya Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Jijini Mwanza (MWAUWASA) na kuiagiza kuandaa mkakati wa kuhakikisha huduma ya maji inaimarika ili kuwanufaisha wananchi wengi zaidi sambamba na kuhakikisha upotevu wa maji unadhibitiwa.

Aidha, ameipongeza Bodi iliyomaliza muda wake kwa usimamizi mahiri wa miradi inayojengwa chini ya MWAUWASA kwenye maeneo mbalimbali yanayozunguka Ziwa Victoria.

Hafla hiyo ya uzinduzi ilihudhuriwa na viongozi mbalimbali akiwemo Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Maji, Mhandisi Anthony Sanga, Wakuu wa Wilaya za Nyamagana, Dkt. Phillis Nyimbi na Dkt. Severine Lalika wa Ilemela pamoja na Wakurugenzi wa Mamlaka za Maji za Musoma, Shinyanga na Sengerema.