News

Posted On: Jun, 12 2020

​Mkutano na Washirika wa Maendeleo wamalizika

News Images

Mkutano na Washirika wa Maendeleo wamalizika

  • Wameipongeza MWAUWASA kwa usimamizi mzuri wa miradi

Wadau wa Maendeleo wanaotekeleza miradi ya maji kupitia programu ya Uboreshaji wa Huduma ya Majisafi na Usafi wa Mazingira ijulikanayo kama LV WATSAN wameipongeza Serikali kupitia Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Jijini Mwanza (MWAUWASA) kwa usimamizi wake mahiri.

Pongezi hizo zimetolewa kwa nyakati tofauti Juni 9 na 10, 2020 na Washirika wa Maendeleo ambao ni Benki ya Uwekezaji ya Ulaya (EIB) na Shirika la Maendeleo la Ufaransa (AFD) katika Mkutano ambao kwa mara ya kwanza umefanyika kwa njia ya Mtandao kutokana na Janga la Virusi vya Corona (Covid 19).

Kupitia mkutano huu wataalam wanaosimamia ujenzi wa miradi iliyo chini ya program ya LV WATSAN hupata fursa ya kuelezea hali halisi ya ujenzi wa miradi, hatua iliyofikiwa, mafanikio sambamba na changamoto zilizopo kwa lengo la kupata ufumbuzi wa pamoja.

Kwa nyakati tofauti wadau hao walieleza kuridhishwa na hatua iliyofikiwa kwenye utekelezwaji wa miradi ambayo baadhi imekamilika na ipo kwenye kipindi cha matazamio na mingine inaendelea kutekelezwa na waliipongeza MWAUWASA yenye jukumu la kusimamia miradi hiyo kwa niaba ya Wizara ya Maji kwa usimamizi mzuri.

Programu ya uboreshaji wa huduma ya Majisafi na Usafi wa Mazingira inatekelezwa katika Jiji la Mwanza, Miji ya Bukoba na Musoma, Miji Midogo ya Misungwi, Magu na Lamadi.