Msako wa wezi wa Maji

Posted On: May 18, 2020


Hivi karibuni, Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa MWAUWASA, Mhandisi Leonard Msenyele na timu yake kwa kushirikiana na Vyombo vya Usalama walifanya msako mkali wa kukamata wezi wa maji.

Tunawafahamisha wadau wetu kwamba msako huu ni endelevu na hatua kali za kisheria zitachukuliwa kwa wote watakaobainika wanajihusisha na vitendo vya wizi wa maji. Ndugu Mteja epuka vitendo hivi ambavyo kwa kiasi kikubwa vinachangia kuzorotesha utoaji wa huduma na vinarudisha nyuma jitihada za Mamlaka za kupanua wigo wa upatikanaji wa huduma.

Chukua hatua, toa taarifa, ushirikiano wako ni muhimu kwetu.

TAZAMA: MSAKO WA WEZI WA MAJI MEI 15, 2020