Preventive maintenance Kona ya Bwiru
Posted On: Mar 08, 2024
Mpendwa Mteja, Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Mwanza (MWAUWASA) inakufahamisha kuwa itafanya matengenezo zuifu (Preventive Maintanance) ya Mitambo ya Kusambaza Maji Kituo cha Kona ya Bwiru siku ya Ijumaa (08/03/2024) kuanzia Saa 2:00 Asubuhi hadi Saa 02:00 Usiku.
Matengenezo yamelenga kuimarisha upatikanaji wa huduma ya maji kwa wateja wanaohudumiwa na mitambo hiyo.
Maeneo yatakayokosa maji katika kipindi cha matengenezo ni pamoja na Kitangiri, Bwiru, Ibungilo, Kawekamo, Lumala, Kiseke, Nyamanoro, Seleman Nassor, Pasiansi, Mondo, Ilemela na Uwanja wa Ndege
Tafadhali kinga maji ili uweze kuyatumia kipindi cha matengenezo.
Imeandaliwa na Ofisi ya Mawasiliano MWAUWASA
07/03/2024
0800110023 (Huduma Kwa Mteja)