TUNASHIRIKI MAONESHO YA NANE NANE

Posted On: Aug 04, 2020


Karibu kwenye Banda la MWAUWASA- NYAMHONGOLOTunayo faraja kubwa kukufahamisha kwamba tunatoa huduma mbalimbali kwenye banda letu la Maonesho katika viwanja vya Nyamhongolo. Miongoni mwa huduma zinazopatikana kwenye banda letu ni pamoja na:

  • 1.Elimu ya taratibu za kujiunga na Mfumo wa Majisafi na Majitaka
  • 2. Elimu ya namna ya kulipa ankara (bili) ya maji kwa kutumia mitandao ya simu.
  • 4. Elimu ya usomaji wa mita
  • 5. Elimu ya ubora wa maji (Namna maji kutoka kwenye chanzo chetu cha Ziwa Voctoria yanavyotolewa ziwani, yanavyosafishwa na kutibiwa kabla ya kukufikia bombani)

Aidha, huduma zingine zinazotolewa katika banda letu ni kutatua kero mbalimbali wanazokabiliana nazo wateja wetu mfano: kutopokea ujumbe wa ankara (bili) ya maji, kubadilisha namba ya simu ya kupokelea ankara (bili) ya maji na pia tunatoa ushauri kwa wateja wetu kuhusiana na matumizi sahihi ya maji ili kuweza kupunguza gharama.

Mbali na haya yote, tunakaribisha maoni ya wananchi wote kuhusiana na uboreshaji wa huduma ya maji kwa ujumla. Karibu tuzungumze.


Baadhi ya wadau waliotembelea bada letu wakipata maelezo kutoka kwa Mtaalam wa MWAUWASA kuhusu namna ambavyo mfumo wa majitaka unavyofanya kazi.Baadhi ya watumishi wa MWAUWASA walioshiriki Maonesho ya NaneNane wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya uzinduzi rasmi wa maonesho hayo kwa Mwaka 2020