TUNZA MAZINGIRA

Posted On: Nov 24, 2023


Ndugu Mwananchi, Mkoa wa Mwanza ni miongoni mwa mikoa iliyoainishwa na Mamlaka ya hali ya hewa Tanzania (TMA) kuwa unatarajiwa kupata mvua kwa kiwango kikubwa cha El-nino katika kipindi hiki cha kuelekea msimu wa Masika.

MWAUWASA inaendelea kuwasisitiza wananchi kuchukua tahadhari kwa kuzingatia kanuni za usafi wa Mazingira hasa katika kipindi hiki cha mvua ili kuepusha hatari ya kutokea kwa magonjwa mbalimbali ya mlipuko.

Tunza mazingira, Jali Afya.

#Usafiwamazingiraniutu 🇹🇿