Ufuatiliaji wa Madeni

Posted On: Mar 08, 2024


Zoezi la ufuatiliaji wa malipo ya huduma za maji kwa Wateja wenye madeni ya muda mrefu linaendelea katika maeneo mbalimbali yanayohudumiwa na MWAUWASA.

Zoezi hili linakwenda sambamba na utoaji wa elimu ya matumizi sahihi ya maji, Utunzaji wa vyanzo vya maji, Ulinzi wa miundombinu ya maji, Umuhimu wa kulipa Ankara (Bili) za maji kwa wakati sambamba na usitishwaji wa huduma za maji kwa wateja wenye wanaodaiwa.

Mamlaka inasisitiza wateja kulipa Ankara (bili) zao za maji kwa wakati ili kuepuka usumbufu wa kusitishiwa huduma ya maji kutokana na Ankara kutolipwa kwa wakati.

#majiniuhai💦