News

Posted On: Jul, 29 2024

WANANCHI 6,378 KUNUFAIKA NA MRADI WA MAJI WA KISIWA CHA BEZI ILEMELA, MWANZA

News Images

WANANCHI elfu 6,378 waishio Katika Wilaya ya Ilemela kwenye Kisiwa cha Bezi Mkoani Mwanza wanatarajia kunufaika na mradi wa maji wa kisiwa cha Bezi ambao unatarajiwa kuanza kutekelezwa mwezi Septemba 2024.

Hayo yamesemwa na Naibu Waziri wa Wizara ya Maji Mhandisi Kundo Mathew alipotembelea na Kukagua Maandalizi ya kuanza kwa ujenzi wa mradi huo wa maji unaotekelezwa na Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Mwanza (MWAUWASA) ambapo ujenzi wake unatarajiwa kuanza Mwezi Septemba 2024 na kukamilika mwezi Februari 2025.

Mhandisi Kundo ameeleza kuwa kazi zitakazofanyika katika mradi huo ni pamoja na ujenzi wa vituo 15 vya kuchotea maji, ujenzi wa tenki la kuhifadhia maji la lita 250,000 na Ulazaji wa mtandao wa mabomba

Kwa upande wake Mbunge wa Jimbo la Ilemela Dkt. Angelina Mabula ameishukru Serikali kwa kuanza utekelezaji wa mradi huo na kusema kwamba mnamo tarehe 22 Aprili, 2024 aliuliza swali la nyongeza bungeni kwa Wizara ya Maji kuwa Lini, Serikali itapeleka huduma ya majisafi na salama kwenye kisiwa cha Bezi.